KILIMO NI UTI WA MGONGO KATIKA DUNIA

             KILIMO NI UTI WA MGONGO


Je ulishawahi kuwaza ingetokea nini kama wanadamu wasingekua wanalima ,wasingekua wanapanda
waishi kama ndege wanavyoishi, waishi kama wanyama wanavyoishi.Je dunia ingekuaje 

Mungu alivyomuumba mwanadamu alimuumba kwa namna ya tofauti kabisa na viumbe wengine.
Mwanadamu ametofautishwa na wanyama vitu vifuatavyo
                  (a)Roho
                  (b)Mwili
                  (c)Nafsi
Leo nataka tuangalie kipengele cha nafsi maana ndani ya nafsi kuna akili,utashi ,uelewa na utambuzi wa mambo ,atawaza avae nini ,ale nini na aishi maisha ya namna gani.
Mahitaji ya msingi ya mwanadamu yapo matatu ambayo ni chakula ,mavazi na malazi,ila hitaji kuu kuliko yote la mwanadamu ni chakula,ndio chakula ni muhimu kwa kila mtu chini ya jua
Hakuna namna nyingine ya kuweza kupata chakula zaidi ya kilimo,ndio maana nikasema na ninawashauri tuungane kuwekeza katika kilimo ili kukomesha janga la njaa katika dunia yetu.Kilimo ni uti wa mgongo kwa wanadamu ,tumeona vita ya urusi na ukraine inavyoathiri maisha ya watu wengi duniani kwa sababu watu wengi hawalimi wala hawajisshughulishi tena na kilimo matokeo yake chakula kinapungua
Wito wangu kwa ulimwengu mzima tuungane kila mmoja tuingie shambani tulime ili kukomesha uhaba wa chakula duniani


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post